Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufunga Maonesho ya Tamasha Kimataifa la Filamu na Sanaa Ndg. Gerson Msigwa akiwa ametembelea banda la COSOTA Desemba 15,2025 Jijini Dar es Salaam .
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (aliyesimama kulia) na Naibu Waziri Uchukuzi Mhe. David Kihenzile wakishuhudia utiaji saini ya makubaliano ya pamoja baina ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania ya matumizi ya kazi za Muziki katika Viwanja vya ndege nchini, anayesaini kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Ndg. Abdul Mambokaleo na kulia anayesaini ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bi. Doreen Anthony Sinare, Januari 13,2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndg. Methuthela Stephen Ntonda kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Meneja Usajili na Kumbukumbu kutoka Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw. Philemon Kilaka akitoa mafunzo ya hakimiliki na umuhimu wa usajili wa kazi za Sanaa na Uandishi kwa Wasanii na Waandishi wa vitabu wa Songea Mjini leo tarehe 27.04.2024. katika semina ya mafunzo kwa wadau hao iliyoandaliwa na taasisi zilizochini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo zinazosimamia kazi za Sanaa nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare akizungumza umuhimu wa kuhuwisha utafiti wa mchango wa Hakimiliki katika Pato la Taifa uliofanyika 2009-2010 kwa ufadhili wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) katika kikao chake na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kilichofanyika Disemba 05,2023 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Gerson Msigwa (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) mara baada ziara yake katika Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam Oktoba 31, 2023, wapili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.Dkt. Emmanuel Ishengoma.
Viongozi wa Taasisi zinazosimamia Miliki bunifu nchini COSOTA, BRELA, BPRA na COSOZA wakisaini makubaliano ya pamoja ya kuanzisha kituo cha kutoa elimu ya miliki bunifu nchini kwa kushirikiana na Shirika la Miliki bunifu Duniani (WIPO) katika hafla ya mgao wa mirabaha, pamoja na utoaji leseni kwa kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha kwa kazi za Muziki kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki ya mwaka 2022 yaliyoliondolea COSOTA jukumu la kukusanya na kugawa mirabaha na kuwaruhusu wabunifu wenyewe kufanya hilo, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare (wa kwanza kulia) akikabidhi Leseni kwa viongozi wa wa Kampuni ya kukusanya na kugawa Mirabaha kwa kazi za Muziki itwayo TAMRISO kufuatia mabadiliko ya sheria ya hakimiliki na hakishiriki iliyotaka wabunifu kukusanya mirabaha yao wenyewe na kujigawia na kulitoa jukumu hilo kwa COSOTA, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda la Afrika (ARIPO) Amadu Bah (kulia) akikanidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha wa msanii Raymond Mwakyusa (Rayvanny) iliyopokelewa kwa niaba yake na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na mdau wa muziki Mhe. Shaban Hamis Taletale, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Bima TIRA Dkt. Baghayo Saqwera (kushoto) akikabidhi hundi ya mfano ya mgao wa mirabaha wa msanii Nasibu Abdul (Diamondplatinumz) iliyopokelewa kwa niaba yake na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Mdau wa muziki Mhe. Shaban Hamis Taletale, katika hafla ya mgao wa mirabaha, Julai 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.