COSOTA YASISITIZA WASANII KUSAJILI KAZI NA KUWA MAKINI NA MIKATABA WANAYOSAINI
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania imeshiriki katika jukwaa la ZUCHU IMBEJU MASTERCLASS kutoa elimu ya hakimiliki kwa vijana chipukizi wanaofanya shughuli za Sanaa ikiwemo Wasanii, Mameneja wa Wasanii, Djs na Watayarishaji wa Muziki.
Mafunzo hayo yamefanyika Juni 23, 2026 jijini Dar es Salaam na yalilenga kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya kazi ya sanaa na kuweza kunufaika na kazi yako.
Katika mafunzo hayo COSOTA imetoa elimu ya hakimiliki kuhusu umuhimu wa mikataba katika utayarishaji na usambazaji wa kazi pamoja na faida za usajili wa kazi.
Akitoa mafunzo hayo Afisa Hakimiliki kutoka COSOTA Bi. Judith Komba amewasihihi vijana hao kuhakikisha wanasajili kazi zao COSOTA ilikuongeza wigo wa masoko na kuweza kunufaika zaidi.
COSOTA imewapongeza wanaandaji wa mafunzo hayo pia imeshukuru kupata fursa ya kutoa elimu ya hakimiliki kwa wadau hao muhimu wa tasnia ya hakimiliki.
Mafunzo hayo yameandaliwa na WASAFI Limited kupitia msanii wa lebo hiyo @officialzuchu pamoja na CRDB bank kupitia IMBEJU.
