Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndg. Methuthela Stephen Ntonda kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2024.
Meneja Usajili na Kumbukumbu kutoka Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw. Philemon Kilaka akitoa mafunzo ya hakimiliki na umuhimu wa usajili wa kazi za Sanaa na Uandishi kwa Wasanii na Waandishi wa vitabu wa Songea Mjini leo tarehe 27.04.2024. katika semina ya mafunzo kwa wadau hao iliyoandaliwa na taasisi zilizochini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo zinazosimamia kazi za Sanaa nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare akizungumza umuhimu wa kuhuwisha utafiti wa mchango wa Hakimiliki katika Pato la Taifa uliofanyika 2009-2010 kwa ufadhili wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) katika kikao chake na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kilichofanyika Disemba 05,2023 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Gerson Msigwa (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) mara baada ziara yake katika Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam Oktoba 31, 2023, wapili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.Dkt. Emmanuel Ishengoma.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro atembelea Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Jijini Dar es Salaam Okoba 10,2023 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi zilizochini ya Wizara yake kwa lengo la kufahamu majukumu .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndg. Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Septemba 27, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 01 Septemba, 2023.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Hakimiliki Tanzania Bw. Victor Tesha (aliyesimama watatu kushoto) na pamoja na wajumbe wenzake mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo, uliyofanyika Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaamu .
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi Cheti cha Utambulisho wa Ubalozi wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania Msanii Barnaba Classic katika hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya COSOTA na Bodi ya Bodi Filamu Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam.