Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YATOA LESENI YA CMO MPYA NA KUHUISHA LESENI ZA CMO MBILI
10 Sep, 2026
COSOTA YATOA LESENI YA CMO MPYA NA KUHUISHA LESENI ZA CMO MBILI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi.Naomi Mungure , ametoa leseni kwa Kampuni ya Tanzania Audiovisual Collective LTD (TAVIC) kwa ajili ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha kwa kazi za Vielelezo vya Kusikia na Kuona (audiovisual works) tarehe 27 Julai 2026,

Aidha, COSOTA imehuisha leseni za Kampuni ya Society of Music Advocacy Limited (SOMA) – kwa ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya kazi za muziki na Kampuni ya Tanzania Reproduction Rights Society Limited (TANRRS) – kwa ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya kazi za maandishi (literary works).

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za COSOTA, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu amezitaka CMO hizo kutekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji, uwazi na weledi, pamoja na kujitangaza kwa wananchi na wadau wa sekta za ubunifu ili viweze kutambulika zaidi na kuwafikia wanachama wengi.

Pia amesisitiza kuwa COSOTA itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa kampuni hizo ili ziweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kuhakikisha kuwa wabunifu wananufaika kutokana na matumizi ya kazi zao .

slot gacor