Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
COSOTA YATOA ZAWADI KWA CISAC
11 Sep, 2026
COSOTA YATOA ZAWADI KWA CISAC

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki COSOTA Bi. Naomi Mungure akimpatia zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la kusimamia watunzi wa kazi za sanaa (International Federation of Authors and Composers Societies - CISAC) Gadi Oron baada ya mkutano wa CISAC Africa Regional Committee (CAF) uliofanyika tarehe 1 na 2 Juni, 2026.
​Pia Bi. Naomi alimpatia Mkurugenzi Mkuu huyo zawadi mbalimbali kutoka COSOTA likiwepo Vazi la Kanga Maalum Kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Kiswahili Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 7 ya Mwezi Julai kila mwaka. Zawadi hiyo ni ishara ya kumwalika katika sherehe za kilele cha siku ya Kiswahili duniani iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Taasisi yake ya Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) itakayofanyika Paris, Ufaransa tarehe 7 Julai, 2026.

slot gacor