KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU WA COSOTA ATEMBELEA BASATA, ASISITIZA USHIRIKIANO WA KUKUZA UCHUMI WA UBUNIFU
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi. Naomi Mungure ametembelea Banda la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika Maonesho ya Mashariki Creative Economy Expo’26, yaliyoandaliwa na Culture and Development East Africa (CDEA) yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi zinazohusika na usimamizi na maendeleo ya sanaa na hakimiliki, pamoja na kujionea huduma na elimu zinazotolewa kwa wasanii na wadau wa uchumi wa ubunifu.
Ushiriki wa viongozi na wadau mbalimbali katika Banda la BASATA unaendelea kuonesha umuhimu wa maonesho hayo katika kuwafikisha wasanii, taasisi na wadau wa sekta ya ubunifu kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kupata elimu na kujenga mazingira bora ya kukuza sanaa na uchumi wa ubunifu nchini.
