MAZUNGUMZO KATI YA COSOTA NA SACEM
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Naomi Mungure afanya mazungumzo na Mkuu wa Maendeleo Kimataifa kanda ya Afrika (International Development Officer Africa) wa SACEM Bw. Akotchaye Okio, SACEM ni taasisi inayosimamia ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha kwenye daraja la muziki.
Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo yaliyopo jijini Paris, Ufaransa.
Kwa kuzingatia uzoefu wa SACEM ambayo ni kampuni inayoongoza kwa ukusanyaji wa mirabaha Duniani ambayo mwaka huu imetimiza miaka 175 toka kuanzishwa kwake ikijivunia matawi 60 duniani na ukusanyaji wa mirabaha takribani dola bilioni mbili za kimarekani.
Kikao hicho kimeangazia fursa za kujengeanauwezo wa kitaalamu pamoja na kuratibu mashirikiano kati ya SACEM na SOMA, kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha kwa daraja la muziki nchini Tanzania.
