Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Hakimiliki Tanzania

To protect the rights of content creators...
PONGEZI KWA CDEA KWA MAANDALIZI YA MASHARIKI EXPRO
11 Sep, 2026
PONGEZI KWA CDEA KWA MAANDALIZI YA MASHARIKI EXPRO

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bi. Naomi Mungure aipongeza Taasisi Cultural and Development East Africa (CDEA)  kwa maandalizi ya jukwaa la Mashariki Creative Economic Expro 2026 kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Taasisi zake.

Bi Mungure ametoa pongezi hizo Agosti 19, 2026 alipokuwa akizungumza katika ufunguzi  wa siku ya pili ya jukwaa hilo ambalo limelenga kusaidiana kutoa elimu ya hakimiliki kwa wabunifu na wasanii pamoja na kuwaunganisha wasanii wa Afrika Mashariki katika kutangaza kazi zao na kupata fursa za masoko.

Aidha Bi. Mungure alishiriki katika mdahalo wa kujadili mikakati ya kuongeza thamani ya kazi za sanaa kupitia matukio ya michezo iliwemo mashindano ya AFCON 2027 yatakayofanyika katika nchi za Afrika Mashariki.

Bi. Mungure alitoa msisitizo kwa wasanii wa muziki wote kujisajili SOMA sababu ndiyo wenye dhamana ya kukusanya na kugawa mirabaha ikiwemo usajili huo ni msingi wa kuhakikisha mapato yaliyokusanywa yanamfikia kila mnufaika. Pia alifafanua usajili wa kazi unafanyika COSOTA.

Akizungumza katika mdahalo huo Prof. Mwakaje alisisitiza umuhimu wa kuimarisha taasisi zinazosimamia sheria na sera za sanaa ili kutoa tafsiri pana ya hakimiliki, Pia alieleza kuhusu maendeleo ya teknolojia yanahitaji mfumo wa sheria unaotambua mabadiliko ya kidigitali (digital enviroment) ili kuhakikisha msanii anpata gawio na thamani halisiya kazi asilia.

slot gacor