UMUHIMU WA KUSAJILI KAZI ZA WABUNIFU
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA). Bi Naomi Mungure(katikati), ametoa elimu ya hakimiliki na umihimu wa kusajili kazi za ubunifu kwa Bw. Abduli Hussein Chacha, marufuku kwa jina la Headmaster_TZ.
Bw. Abduli (kulia) ambaye ni mtayarishaji wa maudhui ya mtandaoni ( Content Creator) na mchekeshaji (Comedian). ametembelea Ofisi za COSOTA kwa lengo la kupata elimu na ufahamu zaidi kuhusu masuala ya hakimiliki pamoja na namna bora ya kulinda kazi zake za ubunifu.
Katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Kumbukumbu na Uzingatiaji COSOTA,Bw. Philemoni Kilaka (kushoto), alitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya usajili pamoja na haki za wabunifu
Akizungumza katika kikao hicho, Bi Naomi amewataka wasanii na wabunifu mbalimbali, wakiwemo watayarishaji wa maudhui ya mtandaoni (Content Creators), kusajili kazi zao COSOTA ili kuziwezesha kupata ulinzi zaidi wa kisheria na kutambuliwa rasmi.
COSOTA inaendelea kutoa elimu kwa wasanii na wabunifu kuhusu umuhimu wa kulinda na kusajili kazi zao, ili kuhakikisha haki zao zinalindwa na wanapata manufaa yanayotokana na matumizi ya kazi zao.
