Msaada wa Kisheria na Utatuzi wa Migogoro
Msaada wa Kisheria na Utatuzi wa Migogoro
Pamoja na majukumu mengine Ofisi ya Hakimiliki kupitia Kitengo cha Sheria inahusika na usuluhishi wa Migogoro mbalimbali inayohusu uvunjifu wa hakimiliki inayoletwa na wanachama katika Ofisi ya Hakimiliki (COSOTA).
Utaratibu wa Kushuhulikia Lalamiko.
1.Mlalamikaji anatakiwa kumwandikia barua Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA kuhusu lalamiko lake dhidi ya mtu binafsi au Taasisi ambayo anaona kwa namna moja ama nyingine imevunja haki zake za kiubunifu.
2. Mara baada ya kupokea barua ya lalamiko idara huandaa barua ya wito kwa mlalamikiwa ili aweze kufika katika ofisi za Hakimiliki kujibu malalamiko dhidi yake ama kumpa muda wa siku zisizopungua saba ili aweze kujibia uhalali wa yeye kumiliki na kutumia kazi husuka.
3.Katika utatuzi wa migogoro ya kazi za wabunifu pande zote hukaa meza moja na maafisa wa sheria na wataalamu mbali mbali wa Hakimiliki ili kusuluhuhisha mgogoro huo,
4.COSOTA uhakikisha pande zote mbili zinamaliza tofauti zao kwa njia ya amani, na iwapo mmoja wao hajaridhika na usuluhishi huo anaweza kwenda mahakamani na COSOTA inaweza kwenda kutoa ushahidi wa kitaalamu.